Sambaza

‘Napiga Kotekote Ilimradi Mkono Uende Kinywani’ – Jux

 

Mkali wa RnB Bongo, Juma Mussa ‘Jux’ ame-sema yeye anapiga kotekote kwani hana timu na hachagui wapi akafanye shoo na wapi asiende, bali anachoangalia ni mkwanja.

Akipiga stori na Ijumaa ShowBiz katika Viwanja vya Posta-Kijitonyama jijini Dar, wikiendi iliyopita baada ya kuangusha bonge la shoo kwenye Wasafi Festival, Jux alisema watu wengi wanamuona mnafiki kwa sababu anaonekana kwenye matamasha ya Wasafi na Fiesta, jambo ambalo linashangaza wengi.

“Mimi ninapiga kotekote, kwa wale ambao wanajua kutafuta pesa vizuri, basi wataelewa ninachofanya. Mimi siyo mnafiki, sina timu, napiga kotekote ilimradi mkono uende kinywani,” alisema akisisitiza anaheshimu pande zote zinazompa mashavu bila kujali tofauti zao kwani hazimhusu.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey