Sambaza

PROMOSHENI YA KING LIMAU NA MARHABA YATINGISHA JIJI LA DAR

Catherine Kahabi (mwenye fulana ya njano) akizungumza na wananchi wa Tandale na kuwaonesha sabuni hizo

Sabuni za za unga za King Limau na Marhaba Soap zinazozalishwa na Kampuni ya Azania Group of Companies ndiyo habari ya mjini kwa sasa!

Gabriel Steven na Catherine Kahabi wakizungumza na wananchi wa Manzese

Leo wakazi wa maeneo ya Manzese, Mabibo, Tandale na Sinza jijini Dar es Salaam, wamepata nafasi ya kujionea wenyewe jinsi sabuni hizo zinavyoongoza kwa kung’arisha nguo, kuwa na harufu nzuri, zisizochubua mikono na zenye uwezo wa hali ya juu wa kuondoa madoa, katika promosheni ya nguvu iliyofanyika mitaani.

Timu ya promosheni katika pichaya pamoja

Katika promosheni hiyo, mamia ya wakazi wa Dar es Salaam wamegawiwa sabuni hizo bure kabisa, huku wakipata maelezo ya namna ya kuzitumia ili kupata matokeo bora kabisa katika usafi wa nguo.

Mabibo Sokoni

“Hizi ni bidhaa mpya, wananchi wengi bado hawajapata bahati ya kuziona sabuni hizi za kisasa kwa hiyo tumezunguka kwenye maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar ili kuwafikia wananchi ambao tunaamini baada ya kusikia maelezo kutoka kwetu na kwenda kuzijaribu wenyewe, watakuwa mabalozi wazuri kwa watu wengine,” amesema Catherine Kahabi, kiongozi wa promosheni hiyo.

Mkazi wa Tandale akifurahia zawadi ya sabuni

“Hizi sabuni ni mpya kwetu sisi watumiaji lakini baada ya kusikia sifa zake, nimepata shauku ya kwenda kujaribu ili nijionee mwenyewe.

Wananchi wa Mabibo Sokoni wakichangamkia fursa

Siku zote huwa napenda vitu bora, naamini sabuni hizi zitakidhi mahitaji yangu,” Neema Salum, mama lishe anayefanya shughuli zake Tandale kwa Mtogole, alisema baada ya kupewa pakiti zake za bure.

Mmoja wa washindi wa papo kwa hapo wa promosheni akiwa na sabuni zake

“Sisi mafundi gereji changamoto kubwa tunayoipata huwa ni nguo kuharibika na kupata madoa sugu kwa sababu ya kazi zetu, si unajua tena!

Mshindi wa maswali ya papo kwa hapo, mkazi wa Mabibo akiwa na sabuni alizojishindia

Lakini kwa maelezo niliyoyasikia leo kwenye promosheni, naamini hizi sabuni zitanifaa sana, ngoja nikazijaribu, Juma Kigeu, fundi gereji maeneo ya Mabibo, naye alisema baada ya kufikiwa na timu ya promosheni za sabuni hizo.

Timu ya promosheni katika pichaya pamoja

Namna ya kujipatia sabuni hizo, ni rahisi sana! Nenda duka lolote lililo jirani na mahali ulipo, usiseme sabuni ya unga bali sema King Limau au Marhaba Soap na muuzaji atakupatia kwa bei nafuu kabisa! Kisha baada ya hapo, nenda kaijaribu mwenyewe na utaona matokeo yake!

Wananchi wa Mabibo wakiwa na nyuso za furaha

 

Wananchi wa Manzese wakichangamkia sabuni

 

Wananchi wa Manzese wakigombea zawadi
Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey