Sambaza

Ruby afunguka mazito baada ya kupigwa na Kusah

“MIMI HUWA SIO MUONGEAJI SANA WA MAMBO MAMBO ILA LEO ACHA BUBU AONGEE ?? .” Hii ni kauli ya Star wa Muziki kutoka Bongo Ruby ambaye kupitia ukarasa wake katika mtandao wa Instagram ameamua kuongea yale ambayo amekuwa akiyapitia kwenye mahusiano yake hasa manyanyaso na kipigo cha mara kwa mara anachopokea kutoka kwa mpenzi wake  Kusah.

Ruby alisema. 

 

View this post on Instagram

 

Nimekuwa nikijiuliza niseme ama nionge kwa nani ila katika hizi dhama lazima kusema ukweli wenda nayopitia ama niliomaliza kupitia yanampata binti wa kike mwenye umri kama wangu au zaidi yangu ila tu amekuwa kifungoni kwa kasumba yakuonekana mbaya kama taswira ilivyo kwa watu wengi kuwa wanawake huwa tunazingua sana. Nimepitia vipigo, manyanyaso, fedhea, kudhalilushwa na kuitwa majina yote kutoka katika kinywa na mikono ya mwanaume ambae alikuja kwangu kutaka support ya kimuziki ila unajua tena love doesn’t ask why? Nilijitolea kumpa support na kuonesha uma kuwa Nina muamini na Nina imani na kipaji chake ila ili hali kuna msemo unasema mwana kulitaka mwana kulipewa; Nimekuwa nikitumia ata jina langu ili dogo kumpambania na kumtambulisha kwa wasanii waliondelea ila mwisho wa siku Nimekuwa nikiambulia vipigo na kuitwa majina ambayo mengine siwezi yaandika kwasababu kuyasema ni kuweka kumbukizi Katika tamati ya maisha niliyomuomba Mungu anipe muongozo na anioneshe njia iliyo bora zaidi. Ukiangalia baada ya kila jambo niliamini labda yataisha na mwenzangu kubadilika ila aikuwa kama nilivyotegemea. Despite kujitoa kwa familia yangu na yake na kuwa mbele kwa kila jambo lake ata kutumia kidogo changu kumpush kwa njia tofauti ila bado aikuwa na mantiki kwake. Mimi ni binti mdogo ambae Nina vision na maisha mbele yangu siwezi katishwa tamaa na jambo lolote linaloendelea na yanayofanywa na baba mtoto wangu kwasababu nimeamua kufikia tamati laasha ningemshauri muda huo anaotumia kuyasema ya uongo angetumia kumuombea mtoto wake akuwe katika njia zimpendezayo Mungu kwasababu kwa kumuangalia sintotaka kumpa mzigo huo kwasababu binafsi anajua nilivyopambana kwake na familia kiujumla ila kwa anayofanya nakuombea Mungu akupe amani ya Moyo. Nimejitahidi kwa uwezo wangu kukuunganisha na kaka yangu @diamondplatnumz mwisho wa siku unishushie makofi natembea nae ukuishia apo unayasambaza na ya mtu tunae eshimiana @juma_jux kusema natembea nae. Hii kama mtoto wa kike inaniharibia taswira mbele ya jamii yangu na watu wanaoniangalia kama kioo ili hali ni chuki tu na kutokujitambua kunafanya mtu anaamua kuunda na magroup kusambaza stori hizi ili nionekane mbaya. INAENDELEA…..

A post shared by Official Ruby ?? (@iamrubyafrica) on

 

View this post on Instagram

 

Pia naomba niombe serikali yangu ya Tanzania kuimarisha adhabu dhidi ya wanaume wanaofanyia wasichana na wanawake vitendo hivi mwisho mahakamani wanapewa faini ya elf 50,000 Au kifungo miezi 6. Mwanaume namna hii anatoka na kuendeleza kuhididimiza jamii na kuzidi kujenga chuki zaidi na zaidi ataendelea kupiga wanawake nje akijua kwamba faini yake ni ndogosana 50,000Tsh Wanawake na wasichana wenzangu ifike muda usidhani kuvumilia vipigo ni mapenzi wala usifikirie kuficha maumivu na haya ndo ustamilivu wa mahusiano ama ndoa kwasababu mwisho huwa sio mzuri na haya ni machache nilioweka wazi kwakuwa sikuwa napost Instagram kuwaonesha Nina mwanaume kamili sana au mzuri sana ila nilifanya kwa kumsupport na kuonesha imani yangu kwake ila malipo yamekuwa fedhea na kuumizwa kiuhalisia. Mimi ni muhanga na nimeiliviuka ili salama basi na wewe usisite kusema na kufikisha sehemu husika kabla tatizo kuwa kubwa. Mungu akasimame na nyinyi kwa kila jambo, MBARIKIWE #RUBYINVISIBLE

A post shared by Official Ruby ?? (@iamrubyafrica) on

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey