Mariah Carey atajwa kama msanii bora wa Kike (Solo Artist) wa muda wote
Kuanzia wimbo wake “Bubbly” wa mwaka 1995 wimbo ambao ulimpeleka namba 1 ya chart za Billboard Hot 100 na kuweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza wa Kike kukamata nafasi hiyo.
Mariah Carey ametajwa na Billboard kama msanii bora wa Kike (Solo Artist) wa muda wote. Carey anazishikilia rekodi za msanii mwenye ngoma nyingi zaidi kwenye namba 1 ya Billboard Hot 100, na msanii aliyekaa wiki nyingi zaidi kwenye namba 1, akiwa amekaa kwa Wiki 79.
Akizungumza baada ya kutangazwa na Billboard, mwimbaji huyo amesema “OMG, kuona mafanikio kwenye chati mbali mbali, kuwasikia nyinyi mkisema hili. Sijawahi kuota kuhusu hii nilipokuwa naanza muziki wangu. Nilitaka tu kuzisikia ngoma zangu redioni.”
Toa Maoni Yako Hapa