Simkumbumbuki Mlela nina mtu mwingine’ – Ebitoke
Muigizaji wa Comedy nchini Ebitoke, amesema kitendo kilichotokea kati yake na msanii Yusuph Mlela, hakikuwa igizo bali ni true love na hawezi tena kumsamehe.
Ebitoke amefunguka na kusema kwasasa ana mtu wake mwingine wa karibu na anafahamiana na kaka yake hivyo hayupo tayari kumkumbuka Mlela.
‘Huyu ni mtu wangu wa karibu, ni rafiki yangu tumefahamiana muda mrefu na haina shida kwasababu anafahamiana pia na kaka yangu, ila kuhusu Mlela siwezi kurudiana naye’, amesema.
Kwa upande mwingine amesema kwasasa anatarajia kuja na Series yake mpya ambayo itaitwa CEO na pia ataendelea kuachia kazi za Comedy kama zamani
Toa Maoni Yako Hapa