Sambaza

Mtoto wa Askofu Maboya: Nyimbo Zangu Zinabadilisha Maisha ya Watu

  Muimbaji wa nyimbo za Injili, Anna Maboya ambaye pia ni mtoto wa Askofu Mkuu wa CAG, Apostle Dunstan Maboya, leo Novemba 17, 2019 amefanya mahojiano kupitia kipindi cha Soul food kinachorushwa na +255 Global Radio na kufunguka mengi.

Kwa sasa Anna anatamba na wimbo wake wa The Battle Is Not Yours aliouimba katika Lugha ya Kingereza akiwa na lengo la kujitangaza zaidi kimataifa.

Watangazaji wa kipindi cha Soul food kutoka kushoto Lucas Masungwa na Gladys Irenza (kulia) wakiwa na Anna Maboya.

 

Nyimbo nyingine za nyota huyo zilizowahi kutamba kipindi cha nyuma ni Hakuna Usiloweza na Sifa ambazo zote aliimba katika Lugha ya Kiswahili, amedai kuwa kinachochangia mafanikio ya kuw ana tenzi nzuri ni ufunuoa anaoupata kutoka kwa Mungu kila anapotaka kutunga na kudai kuwa nyimbo zake ni kama ibada.

Pichani ni wakati Anna akiwa katika studio hizo zilizopo ndani ya Jengo la Global Group, Zinza Mori jijini Dar es Salaam, pia akiwa na watangazaji wa Kipindi cha Soul Food, Glady Sirenza na Lucas Masungwa ambao ndiyo aliofanya nao mahojiano.

Anna amezungumza mengi ikiwemo jinsi ambavyo anatumia nyimbo zake kutangaza neno la Mungu na jinsi ambavyo anapata ufunuo katika kuandika nyimbo zake mbalimbali, akiutolea mfano wimbo wake wa sasa wa The Battle Is Not Yours akisema anaamini utafungua njia kwa watu wengi kuweza kufanya mambo mazuri.


“Kuna watu wengi wapo kwenye wakati mgumu, inawezekana kikazi, kibiashara, kifamilia, ndoa na mambo mengine mengi lakini kupitia wimbo huu wanaweza kubadilika na kutokuwa walewale tena.

“Ulimwengu una mambo mengi, kuna watu wanahitaji faraja tu kuamka na kufanya mambo makubwa, dunia ya sasa watu wengi wanateseka, tumekuwa tukiwapoteza watu wengi kwa kuwa tu hawajapata neno au kauli za faraja, hivyo nyimbo zangu kama huu wa sasa ni tiba na ni huduma nzuri,” alisema Anna katika mahojiano hayo.

Kusikiliza matangazo ya redio hiyo pakua App ya Global Radio katika Android na iOS kwa kuandika 255globalradio

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey