Ben Pol aanika wasanii 15 bora anaowakubali Bongo
Mkali wa muziki wa RnB nchini Tanzania Benard Paul “Ben Pol” ameanzisha mjadala kwa kuweka orodha ya wasanii wake 15 bora wa muda wote kwa kipindi cha miaka 10 hadi 20 mpaka kufikia sasa.
Ben Pol ameweka orodha hiyo ikiwa na majina ya mastaa wa muziki wa BongoFleva kama 1. Ngwair 2. Lady Jay Dee 3. Proffesor J 4. Dully Sykes 5. Juma Nature 6. AY 7. Fid Q 8. Mwana Fa 9. Joh Makini 10. Ben Pol 11. Diamond 12. Mr Blue 13. Ali Kiba 14. Gnako na 15. Nikki Mbishi.
Baada ya kupost hivyo baadhi ya wasanii kama Lady Jay Dee na AY wali-comment kwa kushukuru kuwekwa katika orodha hiyo ya wasanii bora wa Ben Pol.
Ila hali imekuwa tofauti kwa mashabiki ambao wengine walitoa maoni yao kwa kuandika ni sawa wengine walisema haipo sawa ila kwa upande wa msanii wa HipHop Wakazi yeye aliandika kuwa
“Umebeba list nzuri, ingawa naona kama ungeandika 20 badala ya 15, kwa sababu kutoweka watu kama Chid Benz, Jay Moe, TID, Sugu, na Inspekta Haroun haijakaa sawa, ila nakubaliana na orodha hiyo” ameandika Wakazi.
WASANII WANGU BORA KATI YA MIAKA 10 – 20 ILIYOPITA MPAKA SASA:
1. Ngwair
2. Lady Jay Dee
3. Professor J
4. Dully Sykes
5. Juma Nature
6. AY
7. Fid Q
8. Mwana FA
9. Joh Makini
10. Ben Pol
11. Diamond
12. Mr. Blue
13. Alikiba
14. G. Nako
15. Nikki Mbishi— Ben Pol (@IamBenPol) November 18, 2019