Kodak Black huenda akusota jela miaka 30
Baada ya kuhukumiwa miaka 3 siku ya Jumatano, Kodak Black kuongezewa miaka mingine jela.
Mahakama mjini Miami wikendi iliyopita imemshtaki tena rapper huyo kwa makosa mawili ya kumiliki silaha kinyume cha sheria ambapo ni kosa la jinai, na huwenda akahukumiwa miaka 30 Jela kwa makosa yote.
Kwa mujibu wa Miami Herald, kosa moja ni la kununua silaha mwezi January na la pili ni kukutwa na silaha pale alipokamatwa kwenye tamasha la Rolling Loud mwezi Mei.
Toa Maoni Yako Hapa