‘Napitwa na vingi nimeacha kutumia simu’ -Billnass
Rapa Billnass amesema sasa hivi amekuwa anapitwa vingi sana ambavyo vinavyoendelea mitandaoni, kwa sababu ya kuacha kutumia simu mara kwa mara.
Hii inakuja baada ya msanii huyo kusema kuwa hajaiona video ya msanii mwenzake Rosa Ree, iliyokuwa ikimuonyesha akishikwa maungo ya kifuani kwenye mwili wake.
“Mimi muda mwingine napitwa na vitu vingi sana, kwa sababu zamani nilikuwa na tatizo la kuwa “addicted” na simu, muda wote nashika simu kwa hiyo sasa hivi najitahidi na naweza nikakaa siku nzima nikazima simu kwa hiyo muda mwingine napitwa na vitu” amesema Billnass
Billnass ameendelea kusema anafanya hivyo ili kujirudisha katika hali ya kawaida, kwa sababu muda mwingine simu zinaweza zikafanya kazi zisiende na vitu vingine.
Toa Maoni Yako Hapa