Sambaza

‘Nilienda Marekani kuitangaza Tanzania, sio kuiga swaga’ – Young D

Rapa Young Dee amesema hakwenda Marekani kwa ajili ya kula bata na kuiga swaga na “Lifestyle”  ya kule, bali kilichompeleka kule ni kwenda kuwatangazia watu  kuhusu sifa zilizopo Tanzania ambapo mataifa mengine hawana.

 Young Dee amesema anajivunia kuwa mtanzania na kupeleka sifa za Tanzania duniani na kuwaambia kama taifa letu lina amani na halijawahi kumwaga damu.

“Hakuna cha ku-copy Marekani labda nilichokipeleka kutoka Tanzania, Mimi ni m’bongo ambaye nimetokea Dar Es Salaam na kila kitu ambacho tunacho ni baraka, ambazo sehemu zingine za duniani hawana, nilikuwa na kila sababu ya kujivunia kwamba nimetoka sehemu yenye vitu vyote hivi vizuri na kuvipeleka duniani” ameeleza Young Dee.

“Ni vingi sana kama kuwaambia watu kwamba hatujawahi kumwaga damu, kupata uhuru, watu walivyokuwa wakarimu, jinsi ambavyo tuna upendo, naweza kusema nina kila sababu ya kujivunia ya kuwa mtanzania niliyepata nafasi ya kwenda taifa jingine la watu ambao hawako kama sisi” ameongeza.

Ikumbukwe tu rapa Young Dee alikaa nchini Marekani kwa muda wa miezi 6 na sasa amerudi Tanzania na amechia wimbo mpya wa uitwao Jaji mento ambao amewashirikisha Mr Blue na Jay Moe.


Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey