Sambaza

UCHAMBUZI: DIWANI MDOGO ZAIDI TZ NI ‘KICHWA’

Diwani wa kata ya Kijichi Elias Mtarawanje akiwa ndani ya kipidi cha 255FrontPage kutoka +255 Global Radio

Zamani kulikuwa na dhana tofauti ya kuwa huwezi kuwa kiongozi bora kama ukiwa na umri mdogo na uhalisia sio hivyo, Namshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekuja kufanya mapinduzi kwa vijana, kwanza yeye mwenyewe ameonyesha wazi kuwaamini vijana na kuwapa fursa. Hii ni kauli toka kwa Diwani wa kata ya Kijichi Elias Mtarawanje alipokuwa akizungumza leo katika kipindi cha 255FrontPage kutoka @255globalradio ..

…..Mtarawanje akizungumza jambo ndani ya kipindi cha 255FrontPage  kutoka 255 Global Radio

“Kuwa kijana ni kitu kingine na kufanya kazi bora ni kitu kingine, kuwa kijana haikufanyi kuwa bora zaidi; bali ubora wako utaonekana kulingana na utendaji wako, usikivu wako, na nidhamu yako na jinsi gani unafanya kulingana na utaratibu. Vijana huu ni wakati wetu tunahitaji kuonesha jamii kuwa tunaweza kufanya na kuhudumia jamii yetu.” Alisema Mtarawanje.

…Mtarawanje akiwa katika picha ya pamoja na watangazaji wa kipindi cha 255FrontPage Wakwanza kutoka kulia ni Mjomba, Kissa Daniel, Kiraka, Lucas Masungwa na Amos Nyanduku

“Sababu sisi tuna nguvu, tuna uwezo wa kwenda umbali mrefu. Tuwaonyeshe dhahiri wazee waliotuamini kwa kipidi hiki na uaminifu wao kwetu una maana; na hayo yote yanawezekana kwa vijana.” Aliongeza.

Kuaminika kwetu inatakiwa sasa ile imani tulipewa tuionyeshe kwa vitendo.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey