Sambaza

‘Matonya, Dully Sykes wamenilea hadi kufika hapa’- Marioo

MSANII wa muziki wa kizazi kipya Marioo “Toto badi” amenyoosha maelezo na kukata mzizi wa fitina kuhusu kupata msaada kutoka kwa wakongwe wa BongoFleva ambao ni  Matonya na Dully Sykes.

Kwenye baadhi ya mahojiano kati ya Matonya na Dully Sykes, wote wanadai waliwahi kummiliki Marioo kabla hajatoka,  jambo ambalo linachanganya mashabiki kujua Marioo ametokea kwenye mikono ya nani kati yao.

Kwa upande wake Marioo amesema, wote wawili ameshawahi kuishi nao na walimsaidia kwenye maisha yake kama mahitaji ya chakula, sehemu ya kulala na muziki.

“Mimi ni mmoja kati vijana ambao tumehangaika sana kuitafuta hii nafasi, kuhusu Matonya nimepita kwake na tulikuwa na “Producer” Kimambo, nimefanya kazi studioni kwake Biznenga Music, nimeishi kwake na tumeshakula sana misosi ya pale” ameeleza Marioo.

“Lakini Dully Sykes pia nimeshaishi naye na tumeshakula sana vyakula vyake, amenielekeza vitu vingi, tumeshaenda sehemu nyingi, ameshanipa hadi pesa zake, kwahiyo wote ni kaka zangu nawashukuru kwa sifa na heshima zao. Kwahiyo ukimtaja Matonya na Dully kuhusu mimi ni kitu kikubwa” ameongeza

Aidha Marioo ameendelea kusema heshima yake aliyonayo sasa hivi imejengwa kutokana na Matonya na Dully Sykes.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey