Sanchi kupandikiza mimba ya mapacha mwezi ujao
MREMBO mwenye umbo mtikisiko, Jane Rimoy ‘Sanchi’ amesema mwezi ujao ndio anatarajia kwenda kupandikiza pacha watatu nchini Afrika Kusini. Akichonga na Za Motomoto News, Sanchi alisema kwa muda mrefu alikuwa na ndoto ya kufanya hivyo lakini anashukuru muda wake umefika kwa hiyo anatarajia kufanya hivyo mwezi ujao.
“Kila kitu kipo sawa na mpenzi wangu naye ananipa sapoti kubwa kwenye hilo na ndiye nitasafiri naye kwa sababu anajua nilikuwa nikitamani pacha watatu kwa muda mrefu namuomba Mungu tu anisaidie,” alisema Sanchi.
Toa Maoni Yako Hapa