Sambaza

‘The Love Album’ ya Jux yashika namba 2 Album bora ya mapenzi Duniani kwa mujibu wa Audiomack

ALBAMU mpya ya mkali wa RnB Jux ‘THE LOVE ALBUM’ ambayo ina takribani siku ishirini toka itoke rasmi, tayari imeshapiga hatua kubwa na kuwa ni moja kati albamu zinazoongoza kwa kusikilizwa zaidi mtandaoni.

Kupitia mahojiano aliyofanya na kipindi cha Bongo255 kutoka 255 Global Radio Jux alisema “The Love Album imekuwa na records nzuri “Duniani Album yangu ni ya pili kwa kusikilizwa sana kwenye mtandao wa Audiomack, na kwenye mtandao wa Boomplay ni namba 1 kwa Afrika Mashariki.”

Pia aliongeza, “Nilikuwa sijafikiria kutoa album kwababu ya mindset ya nyuma kuwa Album hazifanyi vizuri tena, ila kuna sehemu ukienda watu wanakuuliza kuhusu album yako, Utaona Album ni certificate kwa msanii kujua kama kweli umekua.”

Album hiyo ya Jux ina  jumla ya nyimbo 18 ambapo kuna kolabo nyingi za wasanii kama Diamond Platnumz, Vanessa Mdee, Ruby, Nyashinski na Joh Makini

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey