Sambaza

Aika, Nahreel kutangaza tarehe ya kufunga ndoa hivi karibuni

 

WAPENZI ambao ni wasanii wanaounda kundi la “Navy Kenzo” Aika na Nahreel wamesema hawajahi kuulizwa kama wamefunga ndoa au bado, ila huwa wanaulizwa zaidi ndoa yao itakuwa lini.

 

 

Navy Kenzo, wamesema kwenye mahojiano yao mengi ambayo wamekuwa wakifanya hawajawahi kuulizwa kama wamefunga ndoa au hawajafunga.

 

Nyinyi mtajuaje kama ndoa haipo labda tumeshafunga, halafu hakuna mtu ambaye amewahi kutuuliza hilo swali, watu wanauliza ndoa lini labda kwa sababu hatujaweka mitandaoni ila kwaajili ya Watanzania tutatangaza hivi karibuni tutaweka tarehe na location” wamesema Navy Kenzo.

Wawili hao wamekuwa kwenye mahusiano kwa muda wa miaka 10, tangu walipokutana chuoni nchini India, na wamebahatika kupata watoto wawili wa kiume ambao ni Gold na Jamaika.

 

 

Aidha kundi hilo la Navy Kenzo wamesema wataachia kazi zao mpya kwa mfumo wa “EP”  ambayo itatoka  siku ya Ijumaa ya November 22.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey