Sambaza

Tunda amrushia dongo EX wake

 

Mrembo na Video Vixen Cappuccino Tunda, ameweka wazi ujumbe ambao huwa anatumiwa na aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Casto Dickson, kupitia mtandao wa WhatsApp.

Tunda ameweka ujumbe huo kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram, na ameonekana kukasirishwa na alichokifanya mpenzi wake huyo wa zamani, baada ya kumuongelea kwenye moja ya mahojiano yake. 

Tunda ameandika kuwa “Mimi sio muongeaji na huwa siwezi uswahili kabisa lakini ukiona mpaka nachafua page yangu nakuweka ujue kuna vitu umeshindwa kujiheshimu, huyu kaka sijawahi kuwa na tatizo naye lakini kila kutwa naletewa maneno anayoyaongea kuhusu mimi, wakati kwenye simu yangu halali siku ipite hajanipigia na kuniandikia mesaage” ameandika. 

“Kutwa kupigia watu wangu wa karibu waongee na mimi una hali mbaya, unataka kufa, halafu ukiwa huko unaniongelea ujinga, mtu niliekutengeneza mwenyewe ujulikane leo hii nikuongelee kujibust, unaakili wewe. nakubust navyoongea hivi sema sijali ndiyo nishakuambia sitaki simu zako, sitaki message, tulia kwenye mahusiano yako sahau kuhusu mimi” ameongeza.

Tunda na mpenzi wake huyo wa zamani walikuwa na mahusiano kipindi cha nyuma kabla ya kuachana. Kwa sasa Tunda yupo katika mahusiano na msanii Whozu.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey