Baada ya tetesi za kuwa hana nidhamu; Bright afunguka ukweli wote
BAADA ya kuwepo kwa madai kuwa msanii Bright hana nidhamu na sio mtu wa ahadi za kweli, Bright ameeleza kuwa stori hizo zote ni uongo tu lengo likiwa ni kumchafua.
Bright amejibu hilo baada ya wasanii kadhaa ambao wameshalalamika kwenye vyombo vya habari kutofautiana naye kikazi.
‘Sio kweli ni watu tu wanajaribu kuniharibia bila kujua nimehangaika vipi kuijenga Brand ya Bright ambaye amewekeza muda mrefu’, amesema.
Pia amesema wote wanaolalamika ni wale wanaokwenda kwake kwa kulalamika na hawana hela ya kumlipa kufanya naye kazi lakini anapokuwa hajawapa ushirikiano wao wanachukulia binafsi.
Toa Maoni Yako Hapa