‘Jimbo lipo wazi, natafuta mchumba’ – Isha Mashauzi Afunguka

MUIMBAJI wa muziki wa Taarabu Bongo Isha Mashauzi, amesema anatafuta mume wa kumuoa baada ya kuachika katika ndoa yake ya pili. Muimbaji huyo alisema hayo wakati alipokuwa akifanya mahojiano na kipindi cha Jahazi La Pwani kinachorushwa na 255 Global Radio

“Jimbo liko wazi, nimewahi kuolewa mara mbili mume wangu wa kwanza nimezaa naye mtoto mmoja, na mume wangu wapili hatukubahatika kupata naye mtoto, waume zangu wote tulihitilafiana kila mmoja akaenda kutengeneza maisha yake. Sasa hivi niko mwenyewe natafuta mtu.” Alijibu Isha baada ya kuulizwa swali kuwa kumekuwa na tetesi za yeye kuolewa na waume wa watu.

Aidha aliendelea kwa kusema.“Wanitafute, nahitaji nipate mtu atakayenienzi, atakayenipenda, sijali kuhusu muonekano wake, lakini tu awe na kipato cha kuweza kunisaidia na familia yangu.” Nataka kweli sio kwamba natania, mimi ni mzuri wa kila kitu wanitafute‘ Alisisitza Isha.
