Jibu la Lulu baada ya kutongozwa mtandaoni
MUIGIZAJI wa filamu Bongo Elizabeth Michael (Lulu) amemjibu mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Nasri Mchemwa ambaye alimtumia ujumbe wa kutaka kuwa naye kwenye mahusiano.
Jamaa huyo alitumia mtandao wa kijamii wa Twitter kutuma ujumbe huo wa kumuomba Lulu, awe naye kwenye mahusiano ambapo ameandika kuwa -“umeamkaje Elizabeth Michael Lulu, mzima my love nakusumbua sana ila sio mimi bali ni moyo wangu unasababisha niteseke juu yako kuhusu upendo ulio ndani yangu”
Aidha jamaa huyo ameongeza kuandika “usinione nakutania ni umaskini tu,nilionao ningejitoa kwa vyovyote ili uamini sio utani,nakupenda hadi basi”
Baada ya muda Elizabeth Michael Lulu alikuja kujibu kwa kuandika “Asante Baba” huku akiweka ishara ya upendo.
Toa Maoni Yako Hapa