Sambaza

Nancy Sumari amekuja na ‘Haki’

MISS Tanzania mwaka 2005 na pia majasiriamali Nancy Sumari leo Novemba 27, 2019 amefanya ziara ndani ya kampuni ya Global Group alipokuja kutambulisha rasmi kitabu chake kwenye kipindi maalumu kilichorushwa na +255 Global Radio.

 

 

Katika mahojiano hayo kwenye kipindi maalumu Nancy alisema “Ninayo furaha kubwa na ya kipekee kutangaza ujio wa kitabu changu cha pili cha watoto! Kitabu hiki, kinachoenda Kwa Jina la Haki, ni hadithi iliyotungwa kutokana na sheria ya haki za mtoto ya mwaka 2009, ili kuweza kuwasaidia watoto wa Tanzania kuzijua na kuzilinda haki zao.”

 

 

“Karibuni , pametokea ongezeko la vitendo vya ukatili na ukiukwaji wa Haki za watoto kwa namna nyingi, ikiwemo mimba za utotoni, ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto, na mengine mengi yasiyofaa kwa maendeleo na ustawi wa watoto wetu.” Aliongeza Nancy Sumari

 

 

“Kwa kupitia kitabu hiki cha Haki, ninatarajia kumfundisha mtoto wa Tanzania, kuzijua, kuzitambua na kuzilinda Haki zake, na vilevile kuibua mjadala kati ya watoto, wazazi, walezi, jamii na taifa Kwa ujumla, kuhusu Haki za watoto na namna ambavyo kila mmoja wetu, Kwa nafasi yake, anaweza kubeba jukumu la kuzisimamia pamoja na kuwalinda watoto wetu, katika Tanzania tunayoitaka.” Alimalizia Nancy

 

Miss Tanzania mwaka 2005, Nacy Sumari akimkabidhi kitabu chake kipya cha Haki Meneja wa Kampuni ya Global Publishers Abdalah Mrisho Ofisini kwake.

 

Mhariri Mtendaji  wa Global Publsher  Saleh Ally akiwa na Miss Tanzania mwaka 2005, Nancy Sumari Ofisini kwake alipokwenda kumkabidhi kitabu chake kipya cha HAKI kwaajili ya watoto.

 

Meneja wa +255 Global Radio, Borry Mbaraka akiwa na Miss Tanzania mwaka 2005, Nancy Sumari wakiwa ndani ya studio ya +255 Global Radio baada ya mahojiano na kisha Nancy kumkabidhi kitabu chake kipya cha HAKI

Kitabu cha Haki kitapatikana:

TPH Bookshop – , Dar es Salaam na Dodoma
A Novel Idea – Dar es Salaam na Arusha

Kase Book Store – Arusha
Kupitia namba ya simu – 0759344328 Kwa ajili ya kutumiwa popote ulipo.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey