Deejay Aisher Anayewachezesha Wazungu Bongo Fleva majuu
INASEMEKANA kawaida kuwa kile mwanaume anaweza kufanya, mwanamke pia anaweza kufanya tena ikawa vizuri zaidi. Kuna mwanamke Mkenya anayeamini katika hili hadi kufikia kiwango cha kuingia katika uwanja unaotawaliwa na wanaume kwenye tasnia ya burudani.

Lydia Philly alimaarufu kama Deejay Aisher ni mzaliwa kutoka Migori, nchini Kenya; Ambaye kwasasa anafanya shughuli zake za u’ DJ nchini Ujerumani. Jina la Deejay Aisher limekuwa likikua na kujizolea umaarufu zaidi kutokana na aina ya muziki ambao amekuwa akiucheza kama DJ .

“Niliamua kuwa DJ kwa sababu ya shauku na mapenzi yangu kwenye muziki,” Deejay Aisher alisema katika mahojiano aliyofanya ndani ya kipindi cha Bongo255 kinachoruka kupitia +255 Global Radio.
Aliendelea kwa kusema. ‘Nimekuwa tofauti na DJ’s wengi wa kule kwasababu ya aina ya muziki ambao nimekuwa nikicheza, kuna muziki ukisikika kwa kule Ujerumani wanajua ni mimi kutokana na ustadi na mbinu niwapo kwenye deck.’

Kulingana na Deejay Aisher, ‘DJ mzuri ni yule anayeweza kuchanganya muziki vizuri bila kuvuruga. DJ mzuri pia ana uwezo wa kuchanganya muziki wa aina tofauti na kuwafanya watu waburudike.’ alisema Aisher.
Tangu aanze kuishi nchini Ujerumani toka mwaka 2011 ambapo alienda kwa ajili ya masomo, Deejay Aisher amekuwa akijali zaidi kuupromoti na kucheza muziki wa Kiafrika nchini Ujerumani.

Mwaka huu pekee Deejay Aisher ameshinda tuzo tatu ikiwamo ya Diaspora Night Awards, Tuzo ya DJ bora wa mwaka, na DJ bora Ujerumani. Pia amewahi kushiriki jukwaa moja kufanya back up ya muziki kama DJ na wasanii kadhaa wa Kiafrika, wakiwamo Mr Flavour, Timaya, Kizz Daniel, J Martins, Sauti Sol, Eddie Kenzo, Maleya, Burna Boy pamoja na Diamond Platnumz