Orodha ya wasanii 10 bora wa CNN; Yaleta utata mashabiki wataka Davido asiachwe
Baada ya jina la Davido kukosekana kwenye Orodha ya CNN ya Wanamuziki 10 bora barani Afrika, Mashabiki waikataa orodha hiyo.
Moja ya media kubwa ulimwenguni, CNN hivi karibuni ilitoa orodha ya wasanii wakubwa barani Afrika na majina mengine makubwa katika tasnia ya muziki Afrika.
CNN haikumjumuisha mkali wa muziki kutoka Naija Davido, Badala yake Ikawataja Burna Boy, Wizkid na wasanii wengine katika orodha ya mastaa wakubwa wa muziki barani Afrika
Orodha hiyo iliyotolewa mnamo Novemba 20 na kusahishwa tarehe 26 Novemba, kuna majina yaliongezwa na mengine kuondolewa ili kuendana na orodha yao bora. Mwisho wa siku wakaja na orodha iliyowajumisha wakali wa muziki kutoka Afrika:
Burna Boy,
Angelique Kidjo,
Diamond Platnumz,
Yemi Alade,
Tiwa Savage,
Wizkid,
Mr Eazi,
Shomadjozi,
Busiswa Gqulu, na
Mwila Musonda.
Baada ya orodha hiyo kutoka kumekuwa na muitikio hasi unaoendelea dhidi ya orodha hii kwenye mitandao ya kijamii kwani watu wengi wanaamini haijakamilika kwa kutomtaja Davido.