Sambaza

Rapper Gnawi ahukumiwa kwenda jela kwa kosa la kuwatusi Polisi


MOROCCO; Rapper Mohamed Mounir maarufu ‘Gnawi’ amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa la kutukana Polisi kupitia kipande cha video alichoposti kwenye mitandao ya kijamii.

Hata hivyo rapper huyo mwenye umri wa miaka 31, inadaiwa kuwa kukamatwa kwake kumechochewa zaidi na aina ya kazi zake za muziki, hata baada ya kuachia wimbo wake mpya ujilikanao kama “Aach al Chaab,” aliyowashirikisha Lz3er na Weld L’Griya ambao unazungumzia vitendo vya rushwa Serikalini.

Serikali imekanusha kukamatwa na rapper huyo hakuhusiani na wimbo wake huo bali ni kutokana na video hiyo iliyosambaa mitandaoni inayotusi polisi.

Kwa mujibu wa Al Jazeera reports. Wimbo huo mpya aliyoupa jina la “Aach al Chaab,” ukiwa na maana ya kuwataka watu kuishi kwa muda mrefu ama kuwatakia maisha marefu umetanabaisha wazi wazi maswala ya ukosoaji rushwa, ukosefu wa ajira na unyanyasaji serikalini. Wimbo huo mpaka umekuwa gumzo nchini Morocco na ukizidi kupata watazamaji kupitia You Tube.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey