Kutembea na baiskeli sio kwamba nimefulia ni mazoezi tosha’ – Marlaw afunguka
MSANII wa muda mrefu Bongo Marlaw, amesema ameamua kuwa tofauti kwa kutumia usafiri wa Baiskeli kwenye shughuli zake binafsi na kuachana na usafiri wa Gari, Pikipiki na Bajaji ambavyo wasanii wengi hupenda kutumia.
Marlaw amesema alishamiliki magari makubwa kipindi cha nyuma ila kutembea kwake na baiskeli kunampa mazoezi ya mwili.
“Kitu ambacho kinanivutia kwenye baiskeli ni afya, starehe, burudani na uharaka wa maeneo mengi ya jiji, halafu unatakiwa mtu utokwe hata na jasho kidogo, mimi kama staa jukumu ni vyema kuwajulisha na kuwafahamisha mashabiki kama suala la kutumia Baiskeli lipo vyema” amesema Marlaw
Aidha Marlaw ameongeza huwa anajisikia furaha anapoendesha Baiskeli ila huwa anaangalia na umbali wa safari anayoenda ili kutumia usafiri huo kwa sababu hawezi kwenda nayo umbali mrefu.