Watu wanazusha mtandaoni kuwa tuna bifu, Mimi & Wizkid tupo poa’ – Davido
Davido amefunguka kuwa ni mashabiki ndio wanaobishana na kupeana sumu juu ya uhusiano wake na Wizkid ilihali wawili hao hawana tofauti yoyote kwa sasa. Amesema hayo Davido hivi karibuni kwenye moja ya interview aliyofanya Marekani ambapo yupo kimapumziko.
Davido alisema katika mahojiano kuwa ingawa ni kweli yeye na Wizkid walikuwa katika bifu hapo awali, yote ilisababishwa na wote kuwa wasanii wachanga kwa wakati huo.
Sasa hivi tumekuwa na ni wasanii wakubwa sasa, wote tumeweka mtazamo kupeleka muziki wa Afrobeats mbele zaidi na sio kukaliana kooni kama zamani.
Toa Maoni Yako Hapa