Sambaza

Hii ndio siri ya AliKiba kuwa na sauti nzuri

MSANII wa Muziki wa BongoFleva nchini, Ali Kiba, amesema kuwa nidhamu aliyonayo ndiyo sababu kubwa inayomfanya hadi sasa, kuendelea kuimba nyimbo nzuri zenye kukonga nyoyo kwa mashabiki zake.

Ali Kiba ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Wanafunzi wa Chuo cha Uhazili kilichopo mkoani Tabora, hafla ambayo iliyohudhuriwa na Mkuu wa Mkoa huo, Aggrey Mwanri.

Maisha ya shuleni ni tofauti na mtaani, Shule unafundishwa, mtaani ni kutenda, mtaani muhimu ni nidhamu ili ufanikiwe unachotaka, hata mimi nimefanikiwa sababu ya nidhamu, nidhamu ndiyo imesababisha sauti yangu iimbe vizuri mpaka leo“amesema Ali Kiba.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa huo Aggrey Mwanri amesema “Niwaambie nyinyi wasomi Ali Kiba ni hazina kubwa ya Taifa, nyinyi mnabahati sana kuwa na mtu kama yeye sasa hivi”

Ali Kiba kwa sasa yuko mkoani Tabora, ambapo leo Novemba 30, 2019, anatarajia kufanya Tamasha maalumu ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya #AliKibaUnforgettableTour.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey