Sambaza

Picha: Uni Bash Carnival ya Global Radio ilivyotikisa chuo kikuu Dar es Salaam ‘UDSM’

 

Wanafunzi wa chuo kikuu Dar es Salaam wakiwa kwenye tamasha la Uni Bash Carnival

NOVEMBA 29, 2019, ilikuwa siku ya kihistoria na kiburudani kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu CHA Dar es Salaam (UDSM), baada ya radio ya mtandaoni inayotamba kwa sasa nchini, +255 Global Radio kufika chuoni hapo kuzungumza na wanafunzi hao na kufanya Bonge la tamasha lililopewa jina la Uni Bash Carnival.

…wakimsikiliza mtangazaji wa +255 Global Radio Gabby Mtanzania

Timu nzima ya +255 Global Radio ambao ndio waandaji wa tamasha hilo ilijumuika na wanafunzi wa chuo hicho ikiwa na dhumuni la kuwaburudisha na kuwaelimisha kuhusu mabadiliko makubwa ya teknolojia ya habari na mawasiliano.

Watangazji wa +255 Global Radio wakiserubuka wakati wa ufunguzi wa tamasha Uni Bash Carnival  lililofanyika viwanja vya chuo kikuu Dar es Salaam

Katika Tamasha hilo lililofanyika kwenye viwanja vya chuo hicho huku kukiwa na burudani za kutosha kutoka kwa Ma DJs wakali, zawadi kemkem, wanafunzi hao pia walipewa elimu kuhusu namna ya upatikanaji wa matangazo ya moja kwa moja ya +255 Global Radio ambayo inatumia mfumo wa teknolojia ya mtandaoni kurusha matangazo yake.

Mwanafunzi kutoka chuo kikuu UDSM akipakua Aplikesheni ya +255 Global Radio kwenye simu yake

Sambamba na hayo  +255 Global Radio ilifanikiwa kunadi vipindi vyake vyote vinavyoruka redioni kwa wakati tofauti tofauti ndani ya saa 24 siku 7 za wiki.

Meneja wa +255 Global Radio, Borry Mbaraka akitoa maelekezo ya kupakua Aplikesheni ya +255 Global Radio kwa wanafunzi wa chuo kikuu Dar es Salaam kwenye tamasha la Uni Bash Carnival

Aidha katika tamasha hilo wanafunzi wa UDSM waliweza kufundishwa namna ya kusikiliza kupakua Aplikesheni ya redio kupitia simu zao za mkononi na kompyuta.

Wanafunzi wa chuo kikuu UDSM wakimiminika kwenye tamasha la Uni Bash Carnival

Baadae burudani kali ilishushwa na DJ’s mahiri kutoka +255 Global Radio wakiongozwa na Dj Super, Dj Big Daddy na Dj Obway, sambamba na utambulisho wa watangazji wote wa vipindi kutoka +255 Global Radio chini ya Meneja wao, Borry Mbaraka.

Watangazji wa +255 Global Radio, Gabby Mtanzania (kushoto) na Stewart George (kulia) wakiwa na na mwanafunzi wa UDSM (katikati) wakimkabidhi zawadi ya kitabu cha mtunzi mahiri, Eric Shigongo baada ya kupakua App ya +255 Global Radio.
Wanafunzi kutoka chuo kikuu USDM wakiwa na zawadi zao za vitabu

 

Mtangazi wa kipindi cha Bongo 255 cha +255 Global Radio, Lady Mufasa (kulia) akimkabidhi zawadi ya kitabu mwanafunzi wa UDSM baada ya kujibu swali kwa ufasaha.
Mtangazji wa kipindi cha BONGO 255 cha +255 Global Radio, Stewart George (kushoto) akimkabidhi zawadi ya kitabu cha Eric Shigongo, mwanafunzi wa UDSM baada ya kupakua app ya +255 Global Radio kwenye simu yake.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey