The Game kuacha muziki: Hii ndio zawadi aliyowaachia mashabiki zake
Jayceon Terrell Taylor a.k.a The Game ameiachia “Born To Rap” album yake ya mwisho kwenye maisha ya muziki.
Album hiyo yenye jumla ya ngoma 25 imetoka rasmi November 29 ikiwa pia ni siku yake ya kuzaliwa. Ndani ya album hiyo amevikutanisha vichwa kama; Chris Brown, 21 Savage, Ed Sheeran, Bryson Tiller, Trey Songz, Nipsey Hussle na wengine kibao.
Hii ni album ya 9 na ya mwisho kwa The Game ambaye alianza muziki mwaka 2002. Amefanikiwa kuachia jumla ya Singles 30, Compilation Album 2 na Mixtapes 14.
Toa Maoni Yako Hapa