Sambaza

Kama matusi yatafanya tuheshimiane ni sawa tutakwenda hivyo’ – Barakah The Prince, afunguka

MSANII wa mzuiki wa kizazi kipya Bongo Fleva, Baraka The Prince amesema kuna wasanii wengi wanaotukana sana akiwemo Nay wa Mitego, lakini pia kuna wengine wana matusi mabaya kuliko hata yeye.

Baraka The Prince amesema hayo baada ya kutajwa na mashabiki kama ndiyo msanii, anayeongoza kutukana watu katika mtandao wa Instagram, ambapo amesema mara nyingi hufanya hivyo ikitokea mtu amemkera.

“Mlishakariri hivyo kama ni Baraka tu kuna wengine hata hamuwafuatilii, wanatukana na wana matusi mabaya kuliko mimi, mimi namfikia Nay Wa Mitego kutukana, pia kuna muda wasanii kibao wanatukana lakini likitokeaga kwangu hata kama ni moja watu wanalichukua” ameeleza Baraka The Prince.

Aidha msanii huyo ameendelea kusema “Mimi siyo kama nashindwa kuizuia mihemko yangu ila naishi ndani ya hisia zangu kwa sababu zinafanya niwe huru na amani, ukinikera nakuchana, hutakiwi kukaa na kinyongo mtu akizingua pita naye na kama matusi yatafanya hata tusiheshimiane ni sawa tutakwenda hivyo” ameongeza.

24/7 #Tunakusanua Kinachoendelea Kwenye Ulimwengu Wa Burudani | Kutusikiliza au kupakua app ya radio Bonyeza Hapa http://bit.ly/_255GlobalRadio

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey