Sambaza

Baada ya Wack 100 kusema Nipsey Hussle sio Legend; Meek Mill & TI wamkingia kifua Nipsey

MJADALA umeibuka kuhusu Nipsey Hussle ni LEGEND au sio, hii ni baada ya meneja wa The Game aitwaye Wack 100 kuiambia TMZ kwamba marehemu Nipsey sio Legend kama wengi wanavyompa hadhi hiyo.

“Nipsey ameachia album ngapi? Moja. Hii sio kwamba nazungumza kwa maoni yangu, huu ni ukweli mtupu. Jamaa amefariki akiwa na followers milioni 1, hana hit yoyote kwenye redio, hana platinum yoyote, hana hata ziara yoyote ya muziki. Baada ya kufariki ndio akapiga Platinum na kuuza nakala kibao na kuongeza followers.” Alisema Wack.

Alikuwa ni rapper T.I. ambaye aliibuka na kumjibu Wack 100 kwa kuweka tafsiri ya neno hilo kwenye instagram akaunti yake, amesema LEGEND ina tafsiri nyingi na kwa upande wa Nipsey, inambeba kwenye MCHANGO (impact) yake kwenye jamii

“Mauzo ya ngoma na kuwa na Hit namba 1 sio kipimo pekee cha kuwa LEGEND, Mchango (impact) ndio kitu cha muhimu. Mchango wake haupingiki.” Aliandika T.I. kwenye instagram.


Baadaye aliungwa mkono na Tweets toka kwa Meek Mill, DJ Mustard na wengine ambao waliunga mkono hoja ya Nipsey kuwa LEGEND.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey