Sambaza

‘Sina bifu na mastaa wa kike Bongo karibia wote ni marafiki zangu’- Dimpoz afunguka

 

STAA wa Bongo Fleva Ommy Dimpoz, amefunguka kuwa yeye sio mtu wa kuweka mahusiano yake wazi, pia hana matatizo yoyote na mastaa wa kike Bongo, japokuwa huwa haonekani akiwa nao karibu.

Ommy Dimpoz amesema ana maisha yake ya kawaida na binafsi na kwamba hana chuki na wanawake wa Bongo.

“Nafikiri kuna maisha binafsi na maisha ya kawaida, kuna muda kama msanii unahitaji maisha yako binafsi, halafu mimi sio mtu wa mahusiano yangu kuyaweka wazi, nina upendo wa kutosha na wanawake wote wa Bongo kwa hiyo sina tatizo nao wala siwachukii” amesema Ommy Dimpoz.

Akizungumzia kuhusu kutoonekana akiwa nao karibu na wanawake mastaa Ommy Dimpoz ameeleza kuwa, “Karibia wote ni marafiki zangu na tunashirikiana kwenye mambo mengi, nafikiri ukaribu sio lazima tuwe nao mitandaoni na mimi sijaweka sana kwenye mitandao, lakini tupo poa na vizuri kabisa” ameongeza. 

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey