Sambaza

Mshindi ‘Public Speaking’ Kupewa Tsh Milioni 10

Mkurugenzi wa Global Group, Eric Shigongo,  akizungumza na wanahabari wakati wa uzinduzi wa Shindano la National Public Speaking katika Ofisi za Global Group, Sinza-Mori – Dar es Salaam.

KAMPUNI ya Global Group imetangaza zawadi ya shilingi milioni 10 kwa vijana wa Kitanzania wenye umri wa kati ya miaka 18- 30, wenye ndoto za kuja kuwa wazungumzaji mbele ya halaiki, watakaoibuka washindi katika shindano la National Public Speaking Competition.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Kampuni ya Global Group, zilizopo Sinza Mori jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Eric Shigongo, leo Desemba 4, 2019, amesema washiriki wa shindano hilo, watapata fursa ya kunolewa na waalimu wabobezi wa ‘public speaking’ katika shindano hilo linalotarajiwa kuanza Januari 13, 2020.

Sehemu ya wadau wa tasnia ya Public Speaking wakifuatilia uzinduzi huo.

“Hii ni fursa kwa vijana nchi nzima ambao wana ndoto za kuja kuwa wazungumzaji mbele ya halaiki! Hatuangalii kiwango cha elimu ya mtu kwa sababu wapo wengine ambao hawajasoma sana lakini wana vipaji vya ‘public speaking’.

Anthony Luvanda (wa pili kushoto) akizungumza  katika hafla ya uzinduzi huo.

“Mchujo utafanyika wa kuwapata vijana 30 ambao watapewa mafunzo maalum na baadaye kuchuana vikali, kuwatafuta washindi watatu ambao watajinyakulia zawadi ya shilingi milioni 10, mshindi wa kwanza akipata shilingi milioni 5, mshindi wa pili akipata shilingi milioni 3 na mshindi wa tatu akipata zawadi ya shilingi milioni 2.

Shigongo ameongeza kwamba zawadi hizo ni za mwanzo lakini kuna wadhamini ambao wanaendelea na mazungumzo nao, hivyo uwezekano mkubwa ni kwamba zawadi zinaweza kuongezwa.

Najma Paul akiongea  katika uzinduzi huo.

Kwa upande wake, Lydia Sahani ambaye naye ni miongoni mwa walimu watakaotoa mafunzo kwa washiriki wa shindano hilo.

 

Wadau waliohudhuria  uzinduzi huo wakiwa nje ya Ofisi za Global Group.

Amesema ana imani kubwa kwamba washiriki watakaojitokeza hawatajuta kupewa mafuzo hayo kwani watakuwa kwenye mikono salama ya wataalamu wa kufundisha namna ya kuzungumza mbele ya halaiki.

Paul Mashauri akichangia hoja wakati wa uzinduzi.

Sahani ameongeza kwamba fomu za ushiriki zitaanza kutolewa kuanzia Desemba 10, 2019 hadi Januari 10, 2020 na zitatolewa kwa kiasi cha shilingi 5000/= kwa kila mshiriki katika ofisi za Global Group na kwenye vyuo vyote ambavyo vitatangazwa hivi karibuni pamoja na kwa mawakala wa Global Group waliopo nchi nzima.

Rodrick Nabe akishiriki uzinduzi huo.

Pia washiriki watapata nafasi ya kunolewa na walimu wengine wa Public Speaking wakiwemo mhamasishaji maarufu MC Luvanda, mwanasaikolojia Joel Nnanauka, Paul Mashauri, Chris Mauki na wengine wengi.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey