Sambaza

Nasty C ashtakiwa na uongozi wake wa zamani, wataka abadili jina si mali yake kisheria

KUTOKA nchini Afrika Kusini Rapa Nasty C ashtakiwa na uongozi wake wa zamani Free World Music kwa kukiuka makubaliano ya mkataba akiwa na uongozi wake wa Mabal Noise

Uongozi wa Free World Music unasema kuwa makubaliano kati ya Nasty C na uongozi huo yalikua kama ifuatavyo, Mapato yoyote yatakayoingia kwa Nasty C asilimia 25% yataenda kwa Free World Music, 25% zitaenda kwa Mabala Noise na 50% zitaenda kwa msanii. Lakini Uongozi wa Mabala haukuwahi kupeleka chochote kwenye uongozi huo wa zamani wa Rapa huyo hivyo wanadai fidia ya zaidi ya Milioni 707,019,149.70 za Kitanzania na kumtaka Rapa huyo kuacha kutumia jina jilo la Nasty C

Sakata kama hili lilisha mkuta msanii wa Nigeria Kizzy Daniel ambaye ilimlazimu kubadili jina kutoka Kiss Daniel na kujiita Kizzy Daniel. Nasty C kwasasa yupo chini ya uongozi wa Universal Music Group ambao makao yake makuu ni nchini Marekani .

 

Hii ni kwa ajili yako shabiki wa +255 Global Radio tumekurahisishia kila kilichobora saa 24/7 #Tunakusanua Kinachoendelea Kwenye Ulimwengu Wa Burudani| Muziki Mzuri | Interviews Za Mastaa Unaowakubali| Matukio.. Kutusikiliza au kupakua app ya radio Bonyeza Hapa

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey