Sambaza

Ndoa ya Dada ake Diamond Ilivyoacha Maswali

BAADA ya dada wa msanii nguli nchini; Nasibu Abdul ‘Diamond’, Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’ (34) kuolewa kwa siri, Risasi Mchanganyiko linakupa simulizi ya tukio zima.

Queen ambaye siku za hivi karibuni habari za wambea wa mjini zimekuwa zikidai kuwa ni mjamzito, aliolewa saa tatu usiku wa Disemba, Mosi mwaka huu.

Chanzo kilichohudhuria ndoa hiyo iliyofanyika Mbezi Beach jijini Dar es Salaam nyumbani kwa mume wa dada huyo wa Diamond aliyetajwa kwa jina la Isihaka Mtoro, kilisema:

“Ndoa ilifungwa usiku na mambo yote yalifanywa harakaharaka bila mbwembwe nyingi.”

Akisimulia tukio hilo kwenye runinga ya mtandaoni, Queen alisema aliamua kufunga ndoa hiyo ghafla baada ya mumewe kuamua kulifanya jambo hilo baada ya kutimiza mwaka mmoja wa uhusiano wao

“Tulianza uhusiano Novemba 14 mwaka jana, tulipotimiza mwaka nikashangaa ananipa zawadizawadi kila mara kabla hajapeleka barua kwa mzee Abdul Juma,” alisema Queen.

Mrembo huyo memba pekee wa Wasafi Classic Baby (WCB), alisema kwa kuwa ilikuwa ghafla, ilikuwa ngumu kidogo kwa ndugu zake wa karibu akiwemo Diamond kuridhia, lakini baadaye walielewa.

“Niliweka kwenye grupu la kazini baada ya kuona watu wengi nawapigia hawapokei, baadhi walijibu lakini wengine hawakuona. Nikamtumia meseji Diamond, muda huohuo akanipigia.

Akaomba nimueleze mwenzangu kama anaweza kuisubirisha hadi Jumatano (leo) sababu yuko nje ya nchi na anakwenda kwenye shoo nyingine lakini nikamuomba tu aridhie niolewe, basi akakubali,” alisema.

Aidha, Queen alitumia nafasi hiyo pia kufungukia madai ya kuwa ni mjamzito ambapo alisema si kweli huku akieleza pia ameridhia kuolewa mke wa pili.

“Hata ningekuwa wa nne ili mradi nimeridhia, sikuona tatizo kuolewa mke wa pili. Kuhusu ujauzito hilo si kweli, sina mimba! Nawashukuru kwa kunitakia heri, ikitokea basi inshaallah,” alisema.

Queen alisema wageni waliohudhuria kwenye ghafla hiyo ni ndugu wachache akiwemo mzee Abdul na memba mwenzake wa WCB, Mbwana Yusuph ‘Mbosso’. Kabla ya kuolewa, Queen tayari alikuwa na mtoto mmoja ambaye alizaa na mwanaume mwingine.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey