Sambaza

Je ni kweli Chege alisusia msiba wa Bibi Cheka? Mwenyewe akanusha madai hayo

MSANII wa muziki hapa nchini, Chege Chigunda, amejibu madai ya kususia na kutotoa ushirikiano katika msiba wa Bibi Cheka, aliyefariki hivi karibuni.

 Chege amesema kutokuwepo kwake sehemu yoyote ya mazishi au harusi sio vibaya.

“Watu wameenda wamezika na Chege hakuwepo ila kutokuwepo sehemu ya mazishi, harusi au chochote kile sio vibaya, wala kuwepo sehemu sio wema ila inategemea haukuwepo au  ulikuwepo kwa sababu gani, unaweza ukatokea sehemu ya tukio la umuhimu ila ukawa sio mwema” amesema Chege.

Aidha msanii huyo ameendeleza kusema “Watu wanatakiwa kuelewa hivyo mtu anaweza akatokea sehemu au asitokee, kwanini nisuse siwezi na kuwajibu chochote wanaosema nimesusia msiba, nikijibu nitakuwa sina upeo mzuri wa akili, naamini imani yangu kwanini sijakuwepo inawezekana sikuwepo Dar es Salaam” ameongeza.

Ikumbukwe tu Chege na Bibi Cheka, waliwahi kufanya kazi kwa pamoja katika kundi la TMK Wanaume Family chini ya Mkubwa Fella, lililokuwa na wasanii kama Mh.Temba, KR Mulla, Aslay na wengine kibao.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey