Sambaza

R. Kelly kusota jela akutwa na tuhuma mpya zinazohusisha ndoa yake ya 1994 na Aaliyah

KWA mujibu wa mtandao wa TMZ, waendesha mashtaka wanasema kwamba R. Kelly na watu wake walimpa rushwa mfanyakazi wa serikali ya ‘Illinois’ ili kupata “Kitambulisho feki” kwa ajili ya Aaliyah.

Kitambulisho hicho cha uwongo kilitumiwa kupata leseni ya ndoa iliyoonesha umri wa marehemu Aaliyah’ kama miaka 18. Mmoja ya walokuwa wasimamizi wa ziara za R. Kelly, Demetrius Smith, aliweka wazi mambo yote kupitia Dokumentari ya “Surviving R. Kelly” Kulingana na Smith, Aaliyah alikuwa na umri wa miaka 15 tu wakati huo wakati akiolewa na R. Kelly.

Waendesha mashtaka wanadai kwamba ununuzi wa kitambulisho feki ni rushwa. Na madai hayo yameongezwa kwa shtaka lililopo dhidi ya Kelly huko New York ambalo linamshtumu kwa kuwanyanyasa wasichana kijinsia.

Aidha Katika mahojiano na “Good Morning American” ??mapema mwaka huu, wakili mwingine wa Kelly, Steven Greenberg, alisema Kelly hakujua “Aaliyah alikuwa na umri wa miaka 15 wakati wa ndoa. “Ufahamu wangu ni kwamba hakudai kuwa na miaka 15, ili aweze kuolewa ilibidi asema uwongo juu ya umri wake,” alisema Greenberg.

Fahamu kuwa R. Kelly anashtakiwa katika kesi nne za unyanyasaji wa kijinsia katika eneo hilo. Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 52, bado yuko chini ya ulinzi kulingana na mshtaka yanayomkabili.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey