Sambaza

Rosa Ree asemehewa na BASATA sasa kuendelea na sanaa

BARAZA la Sanaa Tanzania BASATA limemfungulia msanii Rosa Ree kuendelea kufanya kazi za Muziki.

BASATA wamempunguzia adhabu msanii huyo baada ya Novemba 14 mwaka huu kufungiwa miezi 6 asifanye kazi yoyote ya sanaa kutokana na kuachia Video ‘VItamim U’ ambayo ilikuwa haina maadili.

Kutokana na barua ya kuomba kupunguzwa kwa adhabu iliyoandikwa na Rosa Ree, kuanzia leo ameruhusiwa kujishughulisha na kazi yake ya muziki pia anatakiwa kulipa faini ya Shilingi milioni 2 za Kitanzania.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey