Rapper Juice WRLD afariki Dunia
Rapper Juice WRLD, moja ya mwana hip-hop bora wa mwaka aliyekuwa anakuja juu, amefariki ghafla akiwa na umri wa miaka 21.
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ walireport taarifa hiyo jana Jumapili asubuhi (Desemba 8) na kuripoti kwamba Jarad Anthony Higgins a.k.a. Juice WRLD, alikuwa amewasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Midway Chicago akiwa ametokea Los Angeles na kupatwa na Kifafa katika kituo hicho. Alikuwa hai wakati wataalamu wa afya walipofika kwenye eneo la tukio kutoa huduma ya kwanza, lakini baadaye ilitangazwa kuwa amefariki katika moja ya hospitali mjini hapo.
Toa Maoni Yako Hapa