Sambaza

Juma Lukole ampinga Vanessa Mdee kuhusu penzi la Rotimi

Mwanamitandao maarufu nchini Tanzania, Juma Lokole ameipinga kauli ya Vanessa Mdee ya kusema alimgundua mpenzi wake mpya Rotimi kama ndiyo mwanaume wake wa maisha ndani ya siku 2 tu.

Juma Lokole, ameeleza kuwa haamini katika hilo kwa sababu hata kwa Jux alisema hivyo hivyo.

“Mimi siamini katika hilo, huwezi kuanza mahusiano kwa siku mbili, labda ni wale wadada poa wa barabarani kwamba wanakukamata leo halafu wanakuchunguza kama dakika 5 kama una hela au hauna” ameeleza Juma Lukole

Aidha Juma Lokole ameongeza kuwa, “Yale yote ni maneno katika hali ya kurushana roho kwenye mahusiano kila mtu ataongea lake sio kwa sababu kajisemea yeye hata kwa Jux alisema maneno kama hayo ni hali tu ya kawaida” ameongeza.

Kwa sasa Vanessa Mdee, anajiachia nchini Marekani na mpenzi wake Rotimi, huku Jux anatoka kimapenzi na mrembo Nnayika, kutoka barani Asia.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey