Sambaza

Miss Tanzania 2019 ‘Sylivia Sebastian’ atinga 20 bora Miss World

MISS TANZANIA 2019 Sylivia Sebastian ameandika historia na kuipeleka Tanzania kwenye rekodi ya kuingia 20 bora ya nchi zenye vipaji Duniani kati ya nchi 120 zilizoshiriki kwenye mashidano ya urembo ya dunia (Miss World 2019), mara ya mwisho Tanzania kushiriki nafasi hii ilikuwa ni mwaka 1994.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Miss Tanzania wamempongeza Sylivia kwa kuifikia hatua hiyo nzuri kwa kuandika…”KATI YA NCHI 120 ZILOZO SHIRIKI TANZANIA IMO KWENYE 20 BORA ya nchi zenye vipaji duniani kwenye mashindano ya urembo ya dunia MISS WORLD 2019
Hongera sana @syliviasebastian_bebwa hata kwa hapo ulipofikia umetuletea heshima Tanzania kua katika nchi duniani zenye vipaji na Sisi tupo.”

“Miss wajao wamepata pa kuanzia. Na kuendeleza ulipofikia. Umetuweka kwenye Ramani. Umeweka rekodi mpya Mafanikio ni hatua hivyo toka 1994 , 2019 ndio tumefanikiwa kuingia kwenye kipengele hiki cha vipaji. Tunaendelea kukutakia heri kwenye fainali 14 /12/ 2019. Best of luck27 ndio waliofuzu Wakatajwa to 20 na Tanzania tumo.”

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey