Sambaza

Mpenzi wangu akinisaliti siwezi kumvumilia – Uwoya afunguka

  

STAA wa BongoMovie, Irene Uwoya, amesema atakuwa hana noma akimuona mpenzi wake anam ‘kiss, mwanamke mwingine au kumuita majina ya kimahaba, ila kitu atakachokishindwa ni kuona mwenza wake akimsaliti.

 Irene Uwoya, amesema hayo baada ya watu kujaji urafiki wa Wema Sepetu na Aunty Ezekiel, kupeana mabusu hadharani jambo ambalo si la kawaida kwa wanawake kufanya hivyo.

“Mimi naona ni kawaida tu ni watu ambao wana urafiki wa muda mrefu, ku-kiss ni vitu vya kawaida tu hakuna kikubwa hapo haimanishi chochote hata kumwita mtu darling ni sawa tu, hata mimi mtu yeyote naweza kumuita hivyo” amesema Irene Uwoya.

Aidha akizungumzia kuhusu mpenzi wake, kufanya kitendo cha kum ‘kiss’ mwanamke mwingine Irene Uwoya amesema.

“Kwangu mimi mwanaume wangu akimkiss mwanamke itategemea, unajua kuna kiss zinatofautiana ukifanya hivyo katika hali ya urafiki inaonekana na ukifanya katika hali ya mapenzi inaonekana pia, mimi nitachukulia kitu cha kawaida cha urafiki hakuna tatizo  ila akinisaliti siwezi kuvumilia” ameongeza.

 

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey