Sambaza

Marioo atoa ushauri huu kwa wasanii wachanga

MSANII wa Bongo Fleva Marioo, amesema wasanii wachanga wasitegemee msaada kutoka kwa wasanii wakubwa, kwani mastaa hawana muda kabisa na kwamba hata yeye kabla hajatoka, aliwahi kuipitia hiyo hali ya kutaka kusaidiwa na hakupata msaada wowote.

Marioo amefunguka wakati akieleza changamoto zake alizokutana nazo kabla ya kuingia kwenye muziki wa BongoFleva.

“Wasanii wengi walinibania ila kitu ambacho nataka niwaambie vijana wenzangu waliopo mtaani na wanataka nafasi, wasitegemee sana ‘support’ kutoka kwa wasanii kwa sababu wameshasaidia watu wengi ambao wengine wamezingua, hata mimi zamani nilikuwa nakasirika ninapomtumia msanii ujumbe halafu hajibu” ameeleza Marioo.

Marioo ameendelea kusema “Mimi mwenyewe nimeshaumia sana kwenye hayo masuala ya kumpigia msanii simu, halafu anakukatia tena kilichoniumiza zaidi nilimpigia simu mtu ambaye niliamini atanisaidia na ananijua halafu akanipotezea iliniuma sana, ila nimekuja kujua sasa hivi kwamba mastaa wana vitu vingi” ameongeza. 

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey