Sio siri tena! Khloe Kardashian na Tristan Thompson warudiana 100% baada ya skendo ya usaliti
TAARIFA ikufikie kuwa penzi la Khloe Kardashian na Tristan Thompson kurudiana zimethibitishwa na mtandao wa Radar Online.
Chanzo kimoja cha karibu kimeuambia mtandao huo kwamba wawili hao wamerudiana lakini penzi lao linafanywa kwa siri hasa Khloe ambaye ameripotiwa kuogopa watu watamchukiliaje baada ya kuachana na Tristan kwa sababu za Usaliti.
Khloe na Tristan waliachana mapema mwaka huu baada ya Khloe kumfumania baba watoto wake huyo akitoka na Jordyn Woods, rafiki wa karibu na Kylie Jenner.
Toa Maoni Yako Hapa