Sambaza

AY Aiangukia Serikali, Aachia Dude na Rayvanny

Mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Ambwene Yessayah ‘AY’ ameiangukia Serikali, makampuni na watu binafsi akiwasihi kuwekeza zaidi kwenye tuzo za muziki nchini.

 

AY alizungumza hayo leo kwenye mahojiano maalum kupitia Kipindi cha Bongo 255 kinachorushwa na +255 Global Radio.

 

 

AY alisema tuzo hizo zitakuwa ni chachu kwa wasanii kutengeneza muziki mzuri zaidi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

“Tuzo zinaleta hamasa na ushindani, wadau kuanzia Serikali, makampuni na watu binafsi wanapaswa kuona fursa hii.

 

Pia aliwataka wasanii kwenda nje ya nchi na kufanya muziki wa kimataifa ili kupata ladha mpya na kubadilishana uzoefu na wasanii wakubwa duniani.

 

Mkali huyo wa Rap ameachia video ya ngoma mpya iitwayo Distance Remix ambayo amefanya na Jay Rox pamoja na msanii kutoka WCB, Rayvanny.

 

AY amesema wakati akiwa kwenye harakati zake aliisikia ngoma hiyo ikipigwa, hivyo akaipenda na kufanya mawasiliano na msanii aliyeimba ngoma hiyo, Jay Rox ambaye alikubali hivyo wakaingia studio na kuifanya upya.

“Nilikuwa na malengo ya kufanya ngoma kali na kuiachia kabla ya mwaka huu haujaisha, namshukuru Mungu nimefanikiwa na Distance Remix ambayo ina wiki moja sasa inafanya vizuri kwenye platforms mbalimbali za muziki,” amesema AY.

 

Video hiyo imeandaliwa na Director Kenny, mixer amefanya Paul Kruz na producer ni Kenz Ville Marley.

Stori: Steven Kinabo, Dar

 

 

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey