Sambaza

R.Kelly kuonja joto la jiwe tena

KAMPUNI ya LifeTime imetangaza kuja na sehemu ya pili ya filamu (documentary) kumuhusu R. Kelly maarufu “Surviving R. Kelly” ambayo imetajwa kuzinduliwa rasmi kwenye televisheni Januari 3 mwaka 2020.

Filamu hiyo “Surviving R. Kelly Part II: The Reckoning” yenye masaa mawili itaoneshwa kwa siku tatu hadi Januari 5, na itahusisha mahojiano toka kwa wahanga wapya wa vitendo vyake vya Unyanyasaji wa kingono, wanaharakati na watu mashuhuri akiwemo Damon Dash, Mathew Knowles na Jimmy Maynes.

Sehemu ya kwanza ya filamu hiyo ilitazamwa na watu zaidi ya milioni 26 na kuzua mjadala wa dunia. Pia ilipelekea Kellz kupata visanga kadhaa kama kuanzishwa kwa kampeni ya #MuteRKelly pia aliondolewa kwenye Label ya RCA Records.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey