Sambaza

Rapper Tekashi ‘6ix9ine’ aomba radhi kwa jaji kufuatia kesi yake

Tekashi 69 aomba msamaha. Kuelekea hukumu yake wiki ijayo (December 21) rapper huyo ameandika barua kwa Jaji Paul Engelmayer akiomba msamaha na kujutia makosa yake.

Katika barua hiyo iliyodakwa na mtandao wa TMZ, Daniel Hernandez (6ix9ine) ameomba radhi na kusema anastahili nafasi nyingine. Rapper huyo mwenye umri wa miaka 23, amekiri makosa yake na anatumai kwamba maisha yake yatabadilika baada ya kesi hii.

“Nafahamu kwamba maisha yangu hayatakuwa sawa tena lakini natumai mabadiliko haya yatakuwa kwa uzuri tu kutokana na haya yote. Bado najichukulia kama Kioo cha Jamii kwa mamilioni ya watu kama msanii, mtu mashuhuri na binadamu. Ninafuraha kwamba jamii nzima imepata kuniona nikipambana na matokeo ya matendo yangu. Kwa sababu nahisi hii imeleta mwanga kwa yale ambayo yanaweza kutokea kwenye makundi ya Uhalifu.” ameandika Tekashi.

Pia aliongeza kuwa pindi alipokamatwa tu alijihisi ahueni na ameutua mzigo mzito kutokana na makundi ya uhalifu kumuendesha maisha yake kwa muda sasa na ilikuwa ngumu kuweza kujinasua.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey