Sambaza

Cardi B amzawadia mumewe ‘Offset’ Bilioni 1.1 kama zawadi ya birthday

Rapper Cardi B amem-suprise mumewe Offset kwa kumpatia zawadi ya $500,000 sawa na TZS. Bilioni 1.1  mnamo Desemba 14 wakati akitimiza umri wa miaka 28. Kupitia mtandao wa Instagram Card B alishea video wakati akimpatia zawadi hiyo mpenzi wake ambayo iliiweka ndani ya Jokofu (Fridge)

“Kitu gani kingine naweza kumpa mtu ambaye amepata kila kitu? Jokofu!” alisema kabla ya walinzi wake kufungua mlango wa jokofu (Fridge) kuonyesha maburungutu hayo ya dolari yakiwa yamepangwa katika shelfu.

 

View this post on Instagram

 

Little something something for the Birthday boy @offsetyrn ?? Y O U

A post shared by Cardib (@iamcardib) on


Wawili hawa wamekuwa na tabia ya kupeana zawadi za hadhi ya juu. Ikumbukwe Cardi B aliwahi kumnunulia Offset gari aina ya Rolls-Royce Wraith mwaka 2017 wakati alipokuwa akitimiza umri wa miaka 26, pia Offset hakubakia nyuma na yeye mwaka 2018 alimzawadia mpenzi wake Cardi B gari aina ya Lamborghini Urus.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey