Sambaza

Michael Jackson alinipigia simu tumalize bifu na 50 Cent ‘The Game’

RAPPER The Game amefunguka kuwa kipindi ana Bifu na Rapper 50 Cent, Marehemu #MichaelJackson aliwahi kumpigia simu na kumuomba wapatane na wafanye kazi. Amezungumza na HipHopDX.

The Game amesema alipokea simu toka kwa msaidizi wa MJ ambaye walishindwa kuelewana na baadaye aliichukua simu MJ mwenyewe na kumwambia kwamba yeye ni shabiki mkubwa wa ngoma zake na hata album yake (The Documentary) hivyo kugombana na 50 Cent haina maana.

Aliomba wapatane na wafanye naye ngoma moja; “I think that you and Fifty did great work. It would be a travesty if the world never got to hear you guys again. Would you be open to having a conversation and squashing that beef and doing something for my album?” Alisema MJ.

Kitu hicho hakikumuingia vizuri The Game japo hakusema HAPANA ila hakukubali ombi hilo kubwa toka kwa MJ. Amesema kipindi hicho alikuwa anamchukia sana 50 Cent kiasi cha kutamani kumuua.

“At that time I was so in it with Fifty I actually hated Fifty. I wanted to kill him at that time. He probably had the same mutual feelings for me.” Alisema Game.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey