Wahanga wa matukio ya ‘Tekashi 6ix9ine’ watuma ujumbe kwa Jaji; wataka rapper huyo asiachiliwe
Wahanga wawili wa matukio ya Tekashi 69 watuma ujumbe mzito kwa Jaji, wamtaka kutomuachia huru rapper huyo.
Mmoja wa wahanga hao ametoa maelezo kwamba “Tafadhali fikiria kuhusu mimi na maisha yangu unapokwenda kutoa hukumu kwa mtu huyu. Kwanini mtu huyu ambaye karibu ayamalize maisha yangu, aachiwe huru pale tu na mimi ninapokuwa sipo huru tena.”
Tekashi 69 atapandishwa kizimbani katika mahakama ya Manhattan leo kusikiliza hukumu yake ambapo inadaiwa huwenda akaachiwa huru kutokana na ushirikiano aliowapa serikali kwenye kesi hiyo.
Toa Maoni Yako Hapa