Diddy kutunukiwa tuzo ya heshima ‘Salute To Industry Icons’ na Grammy 2020
Sean “Diddy” Combs (a.k.a. Puff Daddy) atatunukiwa tuzo ya heshima iitwayo ‘Salute to Industry Icons’ kwenye hafla ya tuzo za Grammy mwaka 2020 kwa mchango wake mkubwa kwenye kiwanda cha muziki.
Hafla hiyo itafanyika January 25, 2020, usiku mmoja kabla ya tukio maalum la ugawaji tuzo za 62 za Grammy. Wasanii wengine waliowahi kupewa tuzo hiyo kwa miaka iliyopita ni pamoja na David Geffen, Berry Gordy, Lucian Grainge, Jay-Z na mwaka jana ilienda kwa Clarence Avant.
Toa Maoni Yako Hapa